AyoTV

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

on

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania “TFF” limetangaza timu ya Simba ya Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki wa Kimataifa na Sevilla ya Hispania Mei 23,2019 Uwanja wa Taifa, Club ya Simba imetajwa kucheza mchezo huo dhidi ya Sevilla kwa kigezo cha Klabu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika mashindano ya SportPesa Cup kwa timu zinazodhaminiwa na SportPesa.
.
Sevilla waliopo kwenye Ligi Kuu ya Hispania La Liga wataingia Tanzania Mei 21,2019 tayari kwa mchezo huo, Katibu Mkuu wa TFF Kidao Wilfred amesema kigezo kikubwa kilichotumika kuchagua timu ya kucheza mchezo huo ni timu ya Tanzania iliyofanya vizuri katika mashindano ya SportPesa ambapo Simba ilifikia hatua ya nusu fainali.
.
Amesema ratiba ya Ligi Kuu imebana kimetumika kigezo cha mashindano ya SportPesa Cup kumpata muwakilshi wa kucheza na Sevilla, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tarimba Abbas awali kulikuwa na wazo la kuzikutanisha Simba na Young Africans ili kupatikana timu moja lakini ratiba imekuwa ngumu kuzikutanisha timu hizo au kuchezwa michezo mawili.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments