Mwaka wa 2015 umekuwa mwaka poa sana kwa rapper anaeunda kundi la Young Money, Drizzy Drake… baada ya kuisuka list ya Hot 100 Beatles kwa kuibuka kwenye nafasi ya juu zaidi, mafanikio ya rapper huyo yanazidi kuweka headlines baada ya mtandao wa Spotify kumtaja Drake kama ‘most streamed artist of the year‘.
Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard na Spotify wenyewe, kwa mwaka huu wa 2015, Drake amekuwa msanii pekee aliyesikilizwa na watu zaidi ya mara bilion 1.8 mtandaoni na wasikiliaji milion 46!
Latest hitsong yake Hotline Bling, mixtape yake ya If You’re Reading This It’s Too Late pamoja na mixtape ya pamoja aliyofanya na Future; What A Time to Be Alive ndio kazi zilizoongza kwa kusikilizwa zaidi mtandaoni… kwa upande wa wanawake Pop Staa, Rihanna ndio msanii wa kike aliyeongoza kwa kusikilizwa zaidi kwa mwaka 2015 akiwa amesikilizwa zaidi ya mara bilion 1.
Album ya Drake; If You’re Reading This It’s Too Late inashika nafasi ya Album inayosikilizwa zaidi mitandaoni kwa Marekani na wimbo wa Fetty Wap ‘Trap Queen’ unaongoza chati kama wimbo unaosikilizwa zaidi kwenye mitandao.
Billboard imeendelea kuwataja wasanii tano bora kutoka Marekani wanaoongoza kwa kusikilizwa zaidi mitandaoni na wasanii hao ni:
- Drake
- The Weekend
- Kanye West
- Ed Sheeran
- Eminem.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.