Leo January 22, 2018 nikupe hii ambapo vitendo vya kuvamiwa na kushambuliwa kwa askari Magereza vinavyofanywa na wafungwa vimesababisha mgomo wa askari nchi nzima Ufaransa.
Vyama vya wafanyakazi wa Magereza nchini humo vimeapa kufunga magereza hayo leo Jumatatu January 22, 2018 wakishinikiza Serikali kuboresha miundombinu ya magereza na kuongezwa kwa mishahara.
Waziri wa Haki nchini humo Nicole Belloubet ameeleza kuwa serikali itakutana na viongozi wa vyama hivyo ili kusuluhisha migogoro hiyo na kuzuia mgomo huo kuendelea.
Wiki iliyopita inaripotiwa kuwa askari magereza watatu walijeruhiwa vibaya Kusini mwa Ufaransa na kuelezwa kuwa matukio haya yanayotokea kwa mwendelezo kwenye maeneo tofauti tofauti nchini humo.
RC Mjini Magharibi alivyowapokea Wachina kutoka kwa RC Makonda
“Ni aibu kwa kiongozi kukosa ajenda ya kuzungumza” -Mbunge Ditopile