Wateja wa Vodacom Tanzania wameendelea kubadilisha kadi zao za simu katika maduka ya kampuni hiyo Dar es Salaam ili kufurahia mtandao wenye kasi ya 4G ambapo Vodacom Tanzania ilizindua kampeni hiyo Jumatano ya wiki iliyopita na kuibatiza kwa HAPA KASI TU ina lengo la kuwapatia wateja wake huduma ya intaneti yenye kasi zaidi ikijulikana pia kama LTE.
Mbali na kuzindua mtandao wa 4G LTE Vodacom pia imeimarisha mtandao wa 3G ambao unapatikana katika maeneo yote ya miji mikubwa Tanzania, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia aliniambia huu mchongo mpya una kasi ya ukweli na kwa kuanzia itatolewa kwa wateja wote wa Vodacom Dar es Salaam alafu baadae ndio inasambazwa mikoani.
Jinsi ya kubadilisha kadi ya simu kwenda 4G
Mteja wa Vodacom Tanzania atatakiwa kuwa na simu yenye uwezo wa kupata mtandao wa 4G LTE kisha atatembelea duka la Vodacom lililo karibu nae na atapatiwa kadi ya 4G BURE, mbali na kupata kadi hiyo bila malipo mteja pia atazawadiwa kifurushi cha intaneti chenye 4GB BURE.
Baada ya kubadilisha sim card fanya speed test kupitia http://speedof.me/ kushuhudia spidi ya hatari na #Vodacom4G #hapakasitu