Kama bado hujaamua ni wapi unahitaji kuhifadhi pesa zako, au una account yako kwenye Benki ambayo hujaridhishwa na huduma zake, basi una kila sababu kusogelea moja ya Matawi ya Benki ya DTB na iwe ndio mkombozi wako kuanzia sasa.
Ninayo taarifa kutoka Benki hiyo na nimeona uko umuhimu wa kuifikisha kwako pia mtu wa nguvu, kwanza ni kwamba DTB inakuhakikishia huduma mahali popote kwa sababu inafungua Matawi mapya manne kila mwaka ndani ya Tanzania >>> “Mambo mawili muhimu ni kuhusu uuzaji wa Hisa kwa wamiliki wa Benki, ambapo tumefanikiwa kukusanya Bilioni 30 kutokana na mauzo ya hisa hizo… hii imeimarisha mtaji wa Benki, kuwekeza kwenye Matawi mapya, teknolojia na uanzishaji wa huduma mpya“– Hii ni nukuu ya kilichosemwa na Joseph Mabusi, ambaye ni Chief Finance Officer wa Benki ya DTB.
Uthibitisho mwingine ni huu kwamba kila Benki ya DTB inajali kumhudumia kila mtu >>> “Mwaka 2015 tumeweza kuanzisha account za watoto, akina mama, wazee na account maalum kwa ajili ya wanafunzi ambayo tunaiita ‘KISOMI ZAIDI’… Hii inatokana na ukuaji wa Benki kila mwaka” — Joseph Mabusi.
Mengine ya kukufikia ni haya mtu wangu >>> “DTB ina jumla ya miaka 70 tangu imeanzishwa, una kila sababu ya kuiamini… mpaka mwezi wa Septemba 2015, DTB imepata faida ya BILIONI 20, ni ongezeko la zaidi ya 30% ukilinganisha na faida ya mwaka 2014” >>> Joseph Mabusi.
Matawi ya Benki je? >>> “Benki ina matawi 24 Tanzania, kati ya hayo Matawi 10 yako Dar es Salaam… mengine yako Arusha, Mbeya, Mwanza, Kahama, Tabora, Zanzibar, Tanga, Dodoma, Iringa, Mtwara, Moshi na Morogoro… “- Joseph Mabusi
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.