Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ametia saini sheria ya kuongeza umri wa Msichana kutoa idhini ya kufanya mapenzi kutoka miaka 12 hadi miaka 16 ikiwa ni juhudi za kuwalinda Watoto dhidi ya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.
Wanaharakati nchini Ufilipino wamekuwa wakishinikiza kuongeza umri wa idhini tangu miaka ya 1980 kwani sheria ya zamani ililinda ‘Wanyama wanaokula wenzao ‘ na kwamba watoto wa miaka 12 mara nyingi wanaweza kulazimishwa au kutishiwa kunyamaza.
Hadi sasa Ufilipino imekuwa nchi mojawapo katika Nchi ambazo zina umri wa chini kabisa wa ridhaa ya kujamiiana, nyuma ya umri wa miaka 11 wa Nigeria, kulingana na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF).
Chini ya mswada huo ulioidhinishwa na Duterte ambao hauegemei jinsia Mtu mzima yeyote anayeshiriki ngono na Mtu yeyote mwenye umri wa miaka 16 au chini ya hapo atakuwa anafanya ubakaji.