August 22, 2017 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu alifanya ziara katika Wilaya ya Biharamulo ambako alisisitiza juu ya kutekelezwa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo kuwa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi ya misitu kuondoka kabla ya September 9 mwaka huu.
Wakitekeleza maagizo hayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ikiongozwa na DC Saada Malunde, wameteketeza kwa moto nyumba zaidi ya 90 katika hifadhi ya msitu wa Nyantakara eneo maarufu kama “Mombasa Raha” ikiwa ni pamoja na kukamata ng’ombe saba na kuteketeza mashamba yaliyoanzishwa ndani ya hifadhi hiyo.
Meneja Misitu ya Hifadhi wilayani Biharamulo Emmanuel Komba amesema kuwa vijiji ambavyo vinaanzishwa katika maeneo ya mistu bila kufuata taratibu ni kosa kisheria na inaathiri sana uhifadhi na ni sehemu moja wapo ya watu wanaohujumu uchumi wa Taifa.
WANAVYOISHI BUKOBA MWAKA MMOJA BAADA YA TETEMEKO