Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kusikiliza siku nne mfululizo ushahidi wa kesi ya kujihusisha na biashara ya meno ya Tembo inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan na wenzake kuanzia October 17 hadi 20,017. Mbali na Glan, washtakiwa wengine ni Philemon Manase na Salvius Matembo.
Wakili wa Serikali, Paul Kadushi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi imeitishwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi lakini mashahidi hawapo.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Shaidi amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa mfululizo kwa siku nne kuanzia October 17 hadi 20,2017.
MBUNGE LEMA! Kaongea baada ya Polisi kusitisha mikutano yake
https://youtu.be/Blc49WRX2xw