Top Stories

INDIA: Daraja laanguka, 22 wapoteza maisha

on

Leo September 29, 2017 kwenye mji wa Mumbai India, watu 22 wamefariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa, baada ya mkanyagano mkubwa wa watu kutokea mjini hapo wakati daraja moja lilipo poromoka karibu na kituo cha treni.

Waliyoshuhudia wanasema, daraja hilo huenda liliporomoka kutokana mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha wakati huo, hali ambayo iliwafanya watu kukimbilia mahala hapo kujikinga.

Imeelezwa kuwa mara kadhaa mamlaka husika ya miundombinu imekuwa ikilaumiwa kwa kutelekeza miundo mbinu katika mji huo licha ya kuwa mji huo unapokea watu wengi kila siku.

Ulipitwa na hii? KAGERA TENA: Dhoruba nyingine yaangusha nyumba 30

Soma na hizi

Tupia Comments