Leo November 27, 2017 serikali imezindua mkakati wa Taifa wa Kondomu, huku ikielezwa kuwa asilimia 50 ya watu wote nchini hutumia kondomu.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, amesema mkakati umetayarishwa kueleza vipaumbele vinavyohitajika kupunguza maambukizi ya VVU, magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa.
Pia imeelezwa kuwa mkakati huo, unakusudia kuongeza matumizi ya Kondomu kwa wanawake na wanaume kutoka 34% kwa wanawake na 40.5% kwa wanaume ya mwaka 2012 hadi 55% kwa wote ifikapo mwaka 2018.
“Takwimu za matumizi ya kondomu kwa Tanzania ni asilimia 50, matumizi haya yako chini, hivyo kama kondomu zikitumiwa kwa usahihi na mara kwa mara zinauwezo wa kupunguza maambukizi ya VVU.” Waziri Abdallah Ulega
Ulipitwa na hii? Muhitimu wa degree aliyeamua kufanya kazi ya shoe shine
Waliosababishia hasara ya Sh.milioni 370 kwa TCRA wafikishwa Mahakamani