Hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi Namba 441 ya Uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema, Patricia Kisinda amejitoa baada Wakili wa Serikali kusema hawana imani naye kwa kuwa ana urafiki na mke wa Mbunge huyo.
Wakili wa Serikali Sabina Silayo amesema leo July 6, 2017 kuwa hawako tayari kumsomea hoja za awali kwa kuwa hawana imani na hakimu huyo kuendelea kusikiliza kesi hiyo kutokana na kuwa na urafiki wa karibu na mke wa Lema.
Hakimu huyo amekubali kujitoa kwenye kesi hiyo ambayo itaendelea August 8 mwaka huu ambapo atasomewa hoja za awali huku Jalada likipelekwa kwa Hakimu Mfawidhi ili apangiwe Hakimu mwingine.
Hata hivyo, Godbless Lema hakuwepo Mahakamani na Wakili wake Shedrack Mfinanga akidai kuwa anaumwa hivyo kuiomba Mahakama kuahirisha kesi.
Tamko la CHADEMA kukamatwa Mbunge wa Kawe Halima Mdee na viongozi wengine!!!