Baada ya kugundulika Dk. Craig Spencer (33) daktari aliyekuwa akihudumia wagonjwa wa Ebola Guinea ana maambukizi ya ugonjwa huo baada ya kurejea Marekani, nchi hiyo imeweka utaratibu maalum kwa madaktari wote wanaorejea Marekani wakitokea Afrika Magharibi.
Utaratibu ambao umewekwa na nchi hiyo ni ule unaowataka madaktari pamoja na watu wengine wanaotokea ukanda wa Afrika Magharibi waliokuwa wakihudumia waathirika wa Ebola kuwekwa karantini kwa siku 21 kabla ya ‘kujichanganya uraiani’ huko Marekani, ambapo New York na New Jersey wameanza kuutekeleza utaratibu huo.
Zaidi ya watu 8 waliougua Ebola Marekani, ambapo Nina Pham moja ya wauguzi waliopata maambukizi wakati wakimhudumia Thomas Duncan aliyefariki kwa ugonjwa huo, amepona maambukizi hayo na kupata nafasi ya kukutana na rais wa Marekani, Obama ambaye walikumbatiana kitendo ambacho White House imekielezea kuwa ni “namna ya kumsukuru Nina kwa huduma anayojitolea”
Imeripotiwa kuwa mtu wa kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Ebola New York, Dk. Spencer aliyepata maambukizi hayo akiwa Guinea hali yake inaendelea kuimarika.