Taarifa zilizotoka saa kadhaa zilizopita zilionyesha kwamba kati ya Wagonjwa nane waliokutwa na Ebola huko Congo DRC, wawili kati yao wamefariki dunia.
Taarifa hizi zimeendelea kuwashtua na kuwafanya majirani kuzingatia tahadhari ambapo mkuu wa mkoa wa Kigoma Issa Machibya amesema ‘pamoja na tishio la ugonjwa huu kwamba uko DRC Congo lakini DRC ya mbali sana kule kaskazini wanakopakana na Afrika ya kati na Sudan, tumeanza kuchukua tahadhari kwenye mipaka yetu manake binadamu wanatembea na maingiliano ni makubwa’
‘Kuanzia leo nimemuagiza katibu tawala wa mkoa magari yote yenye uwezo wa kubeba vipaza sauti usiku au jioni watu wamesharudi nyumbani yapite kutangazia Wananchi kwa muda wa siku tatu mfululizo licha ya kuweka vipeperushi’ – Machibya.
John Ndunguru ambae ni katibu tawala wa mkoa amesema ‘Kwenye hospitali zetu wameshatenga chumba maalum kama atatokea mgonjwa yeyote manake inabidi Wagonjwa hawa wawekewe kinga au wigo kwa siku 48, vilevile wizara ya Afya imeahidi kutuletea vifaa vya kutosha hasa vya kinga na dawa mbalimbali, tayari maafisa Afya wako hata uwanja wa ndege kukagua kila anaeingia’
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote iwe usiku au mchana iwapo utakua umejiunga na mimi kwa kubonyeza hapa >>> twitter Insta FB