Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr. John Pombe Magufuli, leo December 28, 2017 amekutana kwa mara ya kwanza na kamati maalum aliyoiunda kwa lengo la kuhakiki mali za chama hicho, Ikulu Dar es Salaam.
JPM amewataka wajumbe wa kamati hiyo kufuatilia na kuhakiki mali zote za chama, kumhoji mtu yeyote ambaye atahitajika kutoa taarifa juu mali za chama na kubaini thamani ya mali, mahali zilipo, makusanyo ya mapato na wanaozishikilia ama kutumia mali hizo.
“Nataka mali za chama zikinufaishe chama, nataka mkamhoji mtu yeyote, awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake,” – President JPM
Kwa niaba ya kamati alizungumza Dr. Bashiru Ally ambapo amesema kamati imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi na wote wanaozitumia mali za chama kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa.
“Mwenyekiti katueleza matarajio yake, sababu za kuunda tume hii, faida zake kwa chama na kwa nchi, ametukabidhi vitendea kazi na taarifa mbalimbali na ametueleza kazi yetu ni kuhakiki mali zote za chama,” – Dr. Bashiru
KIKUNDI CHA VIJANA WAZALENDO KIMEZUNGUMZA KUHUSU ALIYOYAFANYA JPM 2017, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA
TAMKO LA MWENYEKITI UVCCM KWA WANAOMSEMA RAIS, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA