Leo July 17, 2019 Nakusogezea stori kutoka nchini Marekani ambapo Muuza dawa za kulevya nguli Duniani El Chapo Guzma amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani pamoja na miaka 30, hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Marekani.
Mahakama ya Shirikisho New York imemkuta El Chapo na hatia katika makosa 10, ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya, utakatishaji fedha.
El Chapo alitoroko gerezani nchini Mexico mwaka 2016 na baadae kukamatwa na kuhamishiwa Marekani.