February 27 2016 Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ilitangaza kuwasimamisha kazi watumishi wake watatu kwa tuhuma za ubadhirifu, Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu Maimuna Tarishi amesema ‘Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ilitangaza Zabuni ya kuchapa vitabu vya kiada vya Darasa la kwanza mwaka 2015 na kampuni ya Yukos Enterprises Ltd ikawa mshindi‘
‘Ufuatiliaji uliofanywa na Wizara katika bohari ambayo ilikuwa ikipokea vitabu hivyo, ulibaini kuwa vitabu vilivyowasilishwa na Kampuni hiyo kwenye Bohari vilikuwa na kasoro‘
‘Kutokana na mapungufu hayo, naagiza kusimamishwa kazi watumishi waliokuwa na jukumu la kusimamia Sheria ya Manunuzi na kazi ya uchapaji wa vitabu, ili kupisha uchunguzi zaidi ‘
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTER FB YOUTUBE