Mkali wa Hiphop, Marshall Mathers aka Eminem ni mmoja kati ya wengi ambao tumewahi kuwasikia kwenye vituko, moja ya story iliyochukua headlines mara ya mwisho ni ile ya beef lake na Iggy Azalea, huyu akasema hivi yule akajibu vile, yakapita!
Hii si taarifa nzuri, hasa kwa kuwaa inamhusu rapper ambaye Dunia nzima inatambua kazi nzuri alizowahi kufanya, inasemekana jamaa time yoyote atafunguliwa mashtaka kwa kesi ya kuiba wimbo wa rapper anayewakilisha kundi la Hotsylz, Raymond Jones.
Jones anadai kuibiwa mashairi na Eminem ambayo ameyatumia kwenye wimbo wa ‘Rap God’ ambao ulikuwemo kwenye albamu ya Eminem ya ‘Marshall Mathers Lp 2′, wimbo una kipande cha sekunde 25 ambacho kimetoka kwenye wimbo wa Raymond unaoitwa Lookin Boy.
Kama ikithibitika kuwa Eminem kafanya kosa hilo, huenda fidia yake ikawa dola mil.8.
Wimbo ambao umeingizwa kwenye madai haya wa Rap God uliingia kwenye vitabu vya rekodi vya Guiness ukiwa umeweka rekodi ya kuwa wimbo wenye maneno mengi kuliko zote ukiwa na maneno 1,560 ndani ya muda wa dakika sita na sekunde nne.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook