Michezo

Nimekusogezea matokeo ya Man City vs FC Barcelona hapa

on

(null)

Michuano ya ligi ya mabingwa wa Ulaya imeendelea leo tena katika hatua ya 16 bora ya michuano ambapo mabingwa wa England, Manchester City waliikaribisha FC Barcelona katika dimba la Etihad katika mchezo wa raundi ya kwanza ya hatua hiyo ya mtoano wa michuano hiyo.

Barca ambao waliitoa City katika michuano hii msimu uliopita, wamefanikiwa kuingiza mguu mmoja ndani kwenye hatua ya robo fainali baada ya kupata ushindi wa 2-1.

Magoli ya FC Barcelona yalifungwa na Luis Suarez katika dakika ya 16 na 30 ya mchezo.

Sergio Aguero aliifungia City goli la kufutia machozi katika dakika ya 69.

Mechi hiyo itarudiwa wiki mbili zijazo katika dimba la Camp Nou ndani ya Jiji la Barcelona.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments