Stori ambazo zimechukua headline hivi karibuni ni pamoja na ripoti ya pili ya madini iliyokabidhiwa kwa Rais JPM ambapo Rais alichukuwa maamuzi makubwa ikiwemo kuamuru baadhi ya viongozi waliohusika kwenye utiaji saini wa mikataba ya madini kuhojiwa.
Leo June 23, 2017 Kituo cha Sheria na Haki za Bainadamu LHRC kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Anna Henga wamezungumza na waandishi wa habari wakitoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa maamuzi makubwa kwenye issue ya madini huku akiikumbusha Serikali mambo 10 ikiwemo kuitaka iwachukulie hatua watu wote waliotajwa katika ripoti za Kamati zote mbili na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma hizo.
Jambo lingine waliloishauri ni kuongeza ushirikishwaji na uwazi katika mambo makubwa yenye maslahi ya Taifa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha Bungeni mikataba inayoingiwa na Serikali kwa ajili ya uchambuzi.
Umnaweza kubonyeza play hapa chini kutazama!!!