Kuelekea michuano ya Mataifa ya Ulaya 2016 (Euro 2016) yatakayofanyika Ufaransa, Chama cha soka barani Ulaya UEFA kimetangaza sheria mpya kuelekea michuano hiyo.Sheria hizo zilizotungwa na UEFA zinahusisha mechi za kirafiki kwa timu za taifa ili kutunza hali ya usalama.
Sheria hizo zimekuja kutokana na hali ya amani nchini Ufaransa kutokuwa nzuri, hivyo ujio huo unaweza kusaidia kupunguza baadhi ya machafuko ambayo hayatabiriki.
Katika sheria namba 21 kipengele cha 4 inasema; Kufuatia mechi ambazo zitakuwa zinahusisha timu ya Ufaransa, haziruhusiwi kucheza mechi za kirafiki ndani ya nchi mwenyeji kabla ya miezi mitatu mashindano kuanza na badala yake ni mpaka mwezi mmoja baada ya mashindano ya mwisho kumalizika.
Sheria nyingine ni namba 21 kipengele cha 5 inasema; Kuelekea fainali ya michuano hiyo kila timu ikiwemo Ufaransa inaruhusiwa kucheza mechi zaidi ya moja ya kirafiki dhidi ya nyingine inayoshiriki michuano hiyo, ikizingatiwa timu hizo zisiwepo kwenye kundi moja la mashindano hayo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.