David Masha ni mtanzania ambaye alipata ajali mwaka 2007 baada yakuomba lift ambapo dereva aliyekuwa anaendesha gari alikuwa amelewa nakuanguka nakumsababishia kushindwa kusimama tena peke yake,lakini amezua gumzo mtandaoni baada yakufunga ndoa na mke wake nakupelekea watu wengi kudai kwamba mke wake alifuata fedha na sio mapenzi kutokana na hali aliyonayo.
David anasema amesoma na mke wake na walikubaliana kuoana muda mrefu na hana fedha kama inavyodaiwa na kwamba harusi yake iligharimu million tisa ambazo alichangiwa na ndugu jamaa na marafiki zake na kwa sasa ameajiriwa kama afisa ustawi wa jamii katika wilaya ya Bumbuli.
“sijampendea david hela hana hela kama wanavyofikiria,miguu yake haikuwa sababu yakusema hapana usiogope mtu Mungu akupi unachokitaka anakupa unachostahili”-Mke wa David