Duniani

Kama wewe ni mtumiaji wa Facebook, tegemea kukutana na mabadiliko haya wakati wowote !!

on

Facebook ndio mtandao wa Kijamii ambao unatumiwa na watu wengi zaidi, Takwimu zinaonesha Duniani kuna jumla ya watu kama Bilioni 7 hivi, alafu Ripoti ya The Statistics Portal 2015 inaonesha watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wako Bilioni 1.96, na kati yao zaidi ya 70% ni watumiaji wa mtandao wa Facebook !!

3d illustration of a facebook logo standing in front of an upright map of the world on a blue reflective surface

Mark Zuckerberg katupasha kuhusu mipango mingine ya Facebook, sasahivi kama ukiandika post yoyote au ukiingia kwenye ukurasa wa mtu yoyote wa Facebook unakutana na alama tatu, alama ya ‘LIKE’, ‘COMMENT’ na alama ya ‘SHARE’… lakini CEO Zuckerberg anasema ni maombi ya muda mrefu watumiaji wa Facebook wanataka iwepo na alama ya DISLIKE, yani kama kitu hujakipenda unabonyeza tu hapo.

1014_mark-zuckerberg-e1413303739290-1940x1091

Mark Zuckerberg, Boss wa Facebook.

Watu wengi wameulizia kuhusu kuwepo alama hiyo, leo ni siku maalum kwa sababu natangaza rasmi kwamba tunashughulikia hicho kitu na muda sio mrefu tutakiweka kwenye majaribio‘ >>> Mark Zuckerberg.

Hiki hapa pia kipande cha Video kinachomwonesha Zuckerberg akiongelea umuhimu wa kuwepo button ya ‘DISLIKE kwenye Mtandao wa Facebook.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments