Rais wa LaLiga Javier Tebas amerudi kwenye headlines baada ya kuomba shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuanza kuifanyia uchunguzi club ya Man City kama kweli haijavunja sheria ya Financial Fair Play wakati wa usajili wake wa wachezaji.
Javier Tebas anaona kuna haja ya Man City anaona kama kuna fedha inatoka Abu Dhabi kuisaidia Man City ambayo inamilikiwa na mwaarabu wa Abu Dhabi lakini pia anaona na PSG ambayo inamilikiwa na mtu wa Qatar anahisi ni hivyo hivyo inakuwa inapewa fedha kinyume cha taratibu.
Kitendo ambacho Javier Tebas anaamini pesa za waarabu zinakuja kuharibu mashindano ya soka barani Ulaya, kama hufahamu kuhusu Financia Fair Play ni sheria ambayo inavitaka vilabu vya Ulaya kujiendesha au kufanya usajili kwa hela inayozalishwa na club.
Kwa maana nyingine kuepusha club kufanya matumizi makubwa kuliko wanachoingiza, sheria ya Financial Fair Play ilianzishwa na UEFA September 2009, hivyo uwepo wa waarabu ambao ni matajiri Javier Tebas anaamini wanavuruga soka la Ulaya kwa fedha zao, Man City na PSG zimekuwa zikifanya usajili wa gharama kubwa.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0