Michezo

Hii ilikuwa jana mashabiki wa Chelsea walipomsukuma mtu kwenye treni (VIDEO)

on

TrainIshu ilikuwa jana, baada ya mechi ya Chelsea na Paris Saint German fans wa Chelsea wakaingia zao kwenye treni kurudi makwao, lakini walifanya kitendo ambacho kilionekana kuwakwaza wengi na hata uongozi wa Club hiyo pia.

Mashabiki hao walimsukuma kumzuia mtu mmoja ili asipande ndani ya treni hiyo huku wakiimba wimbo uliohisisha ishu ya ubaguzi wa rangi.

Wakati wakimsukuma walikua wakiimba nyimbo za kibaguzi zilizolenga kumdhalilisha.

Tutawaadhibu wote waliohusika na kitendo hiki.. kwenye mpira hatuwezi kuruhusu mambo haya, tumepanga pia kuomba wachunguzi kutoka UEFA waweze kutusaidia kuwapata wote waliohusika“-alisema mmoja wa viongozi wa Club ya Chelsea.

Hii ni video wakati mtu huyo akisukumwa na mashabiki hao wa Chelsea.

https://www.youtube.com/watch?v=BgbYBmW1wGY

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments