Mtandao wa kijamii wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.
Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa, nia ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja wake wamebadili tabia ya kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.
Utafiti huo uliohusisha takribani watumiaji 700,000 unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye mtandao huo.
Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.
Hata hivyo Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois, Katherine Sledge Moore, amesema kwa jinsi ambavyo Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.
Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa taarifa ya utafiti huo anasema wanadhani kuwa ilikuwa muhimu kwao kutafiti mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB