Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma amefungua kikao cha Majiji ambapo amewahasa juu ya tabia njema huku akitaja baadhi ya tabia zinazochelewesha utoaji haki ikiwemo uvivu na uchonganishi.
Katika uzinduzi wa kikao hicho siku mbili, Jaji Prof. Juma amesema mahakama ina umuhimu katika jamii na inategemewa kutoa haki kwa kufata sheria na kwamba inatoa haki ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi na kijamii zinapata suluhu za haraka.
“Jambo la tabia ni muhimu sana kuhakikisha tunajenga, kwani uelewa tunaweza kujiendeleza lakini tabia tunajifunza kutoka kwa wenzetu.Mifano ya tabia inayofanya tusitoe haki kwa wakati ni Uvivu, Uchonganishi, Ulalamishi, Kuchelewa na Ubishi usio na mpango,“alisema.