Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya habari zilizoandikwa kwenye magazetini hii kwenye gazeti la Mtanzania yenye kichwa cha habari ‘Facebook sasa kutuma na kupokea fedha bure’
#MTANZANIA Siku chache zijazo kupitia App ya Messenger watumiaji watafanya malipo ya bidhaa, kutuma na kupokea fedha pic.twitter.com/XIeROSEDrp
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
Gazeti hilo limeandika kuwa utandawazi unazidi kushika kasi ambapo kadri siku zinavyozidi kwenda mambo yanabadilika. Ndiyo maana sasa hivi kuna mambo mengi ambapo licha ya kuwa Tanzania mambo mengine yanachelewa kutufikia, lakini siku moja tutatumia huduma hizo kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea kiteknolojia.
Kila kukicha mmiliki wa mtandao huo, Mark Zurgbeck amekua na mawazo mapya ya kuvutia kwa wateja kwenye huduma yake hiyo kwa kubuni mambo mbalimbali yanayowagusa wateja wake.
Kama wewe ni miongoni mwa wanaotumia mtandao huu kupitia App ya Messenger tambua kuwa siku chache zijazo utakua na uwezo wa kufanya malipo ya bidhaa au kutuma na kupokea fedha kupitia mtandao huo.
Huduma hiyo iliyobatizwa jina la PayPal itakua ikitumika kama ilivyo ile ya simu japo cha kufurahisha hapa ni kuwa huduma hiyo haitakuwa na makato ya aina yoyote kama ilivyo kwa mitandao ya simu, isipokuwa tu itawahusu watumiaji wa Debit Card pekee na walio na umri wa miaka 18 na kuendelea.
Huduma hiyo itaanza kutumika nchini Marekani ambapo mtu atatuma na kupokea fedha huku ikitarajiwa kusambaa kwenye mataifa mengine.
Namna ya kutumia huduma hii fungua sehemu yako ya Chatting kisha chagua More halafu nenda kwenye alama ya $ halafu nenda palipoandikwa ‘Pay’ kisha unamalizia na sehemu iliyoandikwa ‘Add New Debit Card kisha utaulizwa kiasi unachohitaji kulipia utaingiza na kuletewa risiti inayoonyesha kuwa malipo yamekamilika.
Source: Gazeti la Mtanzania
#RaiaTANZANIA Urusi imetoa fursa kwa wahitimu kidato cha sita watakaopata daraja la kwanza kusoma bure udaktari pic.twitter.com/Zzk1GWrDSx
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#RaiaTANZANIA Mwanafunzi Kenya ajitia Kitanzi kwa kupoteza dau la Sh 80000 aliloweka ktk mechi za Euro 2016 pic.twitter.com/sLeR3FjMCf
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#RaiaTANZANIA Wajawazito Zahanati ya Sibwesa Katavi wajifungulia chumba kimoja kinacholaza wagonjwa mchanganyiko pic.twitter.com/2IKJcikqzl
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#NIPASHE Ajali ya mabasi ya City Boys yakatiza ndoto ya Sangoma baada ya kuvunjika mkono na kuchomoka nyonga ya mguu pic.twitter.com/VtuA7JOztT
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#NIPASHE Madini yachangia 3.5% ya pato la Taifa, pamoja na kuziwezesha jamii zinazozunguka migodi kunufaika pic.twitter.com/NYMQDJG4VP
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#NIPASHE Wawekezaji wa nje waalikwa ktk sekta ya gesi, mafuta, umeme na vipuri ili watanzania waweze kunufaika pic.twitter.com/eqUX1vI33W
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#NIPASHE Bomba la mafuta Uganda-Tanga litafanya kazi miaka 27 bila kusimama hata kama kiasi zaidi hakitagundulika pic.twitter.com/BZqvWsDzSb
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#NIPASHE Baadhi ya wauza mafuta Arusha walalamikia wateja wanaodai risiti wakisema 'wanawachinjia baharini' pic.twitter.com/QHRznoKvr3
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#NIPASHE Shule 14 kati ya 15 zilizojengwa kwa nguvu za wananchi Simiyu zanyimwa usajili kwa kukosa vigezo pic.twitter.com/gvxTrF1spr
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#NIPASHE Mameya wawili wa zamani wa Rwanda wafungwa maisha kutokana na mchango wao ktk mauaji ya Kimbari mwaka 1994 pic.twitter.com/zanZU0Kd35
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Katiba imetoa mamlaka ya ukaguzi wa hesabu kwa CAG lakini inaonyesha Wizara ya fedha inamhakiki pia pic.twitter.com/QwlePYtCa9
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Sheikh Ponda Issa Ponda amempongeza Rais Magufuli kutokana na ahadi yake ya kurejesha mali za Waislamu pic.twitter.com/dUsu1umZOY
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Wastani wa Watanzania tisa wanafariki kila siku kutokana na ajali zinazosababishwa na vyombo vya usafiri pic.twitter.com/bcXhwEA4GB
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Uturuki kuleta wawekezaji nchini, kujenga viwanda vya dawa hatua ambayo itapunguza uagizaji wa dawa nje pic.twitter.com/pleCY2otFu
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Bodaboda waendelea kumtega RC Makonda, wakiuka agizo alilolitoa la kuwataka wao na abiria kuvaa kofia pic.twitter.com/bMfug8E2rk
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Serikali imeiagiza DAWASA kuhakikisha inawafikia wateja 400,000 ifikapo July mwakani pic.twitter.com/nGE9KQGhse
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Serikali imeiagiza DAWASA kuhakikisha inawafikia wateja 400,000 ifikapo July mwakani pic.twitter.com/nGE9KQGhse
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Serikali yasema haiwezi kuruhusu Tanga kuwa kichaka cha ujambazi kwa kuwa ni eneo la kimkakati wa uchumi pic.twitter.com/WNxikVe2vf
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MWANANCHI Askari mmoja Marekani amemuua kwa kumpiga risasi mtu mweusi wakati akinyoosha mkono kuchukua leseni pic.twitter.com/4oG4GnB2kT
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MTANZANIA Benki zakomaa kutoza VAT, wasema haikwepeki lazima mteja achangie na ndio maana halisi ya VAT pic.twitter.com/svylch8YdH
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#MAJIRA Kaburi la mtu wa ajabu lagundulika Tanga inadaiwa alikuwa na nguvu za pekee akiita mtu inasikika umbali km 1 pic.twitter.com/ENainfBfE1
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#HabariLEO Gereza la Songwe kuhamishwa ili kupisha shughuli za uchimbaji madini ya niobium yaliyogundulika eneo hilo pic.twitter.com/BD0hEQj7Jc
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#HabariLEO Kusumbuliwa na tumbo kwamnusuru na kifo kwenye ajali ya City Boy, alishuka muda mfupi kabla ya ajali pic.twitter.com/5FaCfSBNQZ
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
#HabariLEO TANESCO: Wateja ambao mita za LUKU zipo ndani watoe taarifa ili zitolewe nje lengo ni kurahisisha ukaguzi pic.twitter.com/xUK0bUZ6Vw
— millardayo (@millardayo) July 8, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 8 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUTAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI