Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, leo December 14, 2017 imemuachia huru Naibu Meya wa zamani wa Jiji la Arusha na Diwani wa sasa wa Kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe (Chadema) kwa kukutwa hana hatia.
Msofe ameshinda keshi ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha upotevu wa kiasi cha Tsh Mil 8 ambazo ni fedha za Halmashauri ya Jiji la Arusha. Diwani huyu alifikishwa mahakamani hapo na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mnamo September 23, 2016.
Alifikishwa mahakamani hapo na mwenzake ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Daraja Mbili, Modestus Lupogo na kusomewa makosa matatu likiwemo la kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume cha sheria.
Akisoma hukumu hiyo leo, Hakimu Gwanta Mwankuga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, amesema kuwa amepitia hoja za mashahidi wa pande zote mbili na kubaini kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka uliokuwa na mashahidi watatu haukuwa na mashiko kuishawishi mahakama hiyo kuweza kuwatia hatiani washtakiwa.
Wanawake waliovishana pete ya uchumba Mwanza Mahakamani tena