Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemwambia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kuwa anaewasukuma ndani wote wanaoharibu mazingira na amesema yupo tayari kupokea maelekezo mapya katika kusimamia mazingira.
“Hawa jamaa huwa nasukuma ndani halafu nawafyekelea mbali wanasema ameletwa mbabe mi nafanya kwa kutii maelekezo ya sheria, nisaidie mkuu wangu mimi ni Mkuu wa Mkoa wa 21 kilio changu hii Tabora isije ikafia mikononi mwangu” RC Mwanri