Wiki iliyopita serikali ya Zimbabwe ilitoa ruhusa kisheria bangi kulimwa kama mazao mengine ya chakula au biashara.
Ruhusa hiyo imetolewa ili zao hilo litumike kwa ajili ya matibabu. Kwa watakaotaka kulima zao hilo, watapewa leseni ya miaka mitano itakayoruhusu kumiliki, kusafirisha na kuuza bangi na bidhaa zake zilizokaushwa.
Leo Ayo TV na millardayo.com inakuletea nchi nne ambazo wananchi wake wana matumizi makubwa ya bangi zaidi ya nchini yoyote duniani.
Lesotho
Kilimo cha bangi nchini humo kinatajwa kuwa ni kama cha mazao mengine kama mahindi kwaajili ya matumizi ya dawa na husafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini.
Inaelezwa kuwa miaka ya 2000 takribani asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini ilitoka nchini Lesotho.
Afrika Kusini
Mwezi April 2017, Afrika Kusini ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi ya nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa.
Matumizi ya bangi nchini humo bado ni kinyume na sheria, mpaka pale sheria itakapobadilishwa na kuruhusu wafanyabiashara walime na kuwekeza kwenye kilimo cha bangi.
Ghana
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaitaja Ghana kuwa ya tatu duniani kwa matumizi ya bangi ambapo asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanavuta bangi.
Hatahivyo bangi ni haramu nchini Ghana japokuwa kumekuwa mijadala ya kitaifa kuomba sheria kuhalalisha bangi nchini humo mamlaka zimeeleza kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.
Korea Kaskazini
Matumizi ya bangi Korea Kaskazini haichukuliwi kuwa kinyume na sheria na hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha na kuuza bangi nje ya nchi ili kupata fedha za kigeni.
Bangi Korea Kaskazini inauzwa kwenye maduka ya vyakula na watu huvuta bangi popote bila kificho.
Mapokezi ya Serengeti Boys baada ya kuwasili Tanzania na Kombe