Leo March 2, 2018 nakusogezea hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo imemuhukumu Raia wa China, Liu Xiu Feng jela miaka 20 ama kulipa faini ya Shilingi Milioni 110 baada ya kukiri kosa la kukutwa na Meno ya Simba mawili.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kueleza kuwa mshtakiwa huyo amekiri kosa.
Hakimu Shaidi amesema kuwa kutokana na mshtakiwa huyo kukiri kosa mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka 20 ama kulipa faini ya Tsh.Mil 110.
“Unahukumiwa kwenda jela miaka 20 ama ulipe faini ya Shilingi Milioni 110,” Hakimu Shaidi.
Baada ya kutolewa hukumu hiyo, mshtakiwa Feng aliepuka kwenda jela baada ya kulipa faini hiyo ya Shilingi Milioni 110.
Raia huyo wa China alikabiriwa na kosa la kukutwa na Meno mawili ya Simba katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Inadaiwa alikutwa na Meno hayo February 7,2018 ambapo yanathamani ya Shilingi Milioni 11, 029,900.
Naibu waziri alivyomfungia Roma leo na kumpa onyo Nay wa Mitego