Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo January 8, 2018 imeeleza kuwa kwa mwezi July hadi December kwenye Mwaka wa Fedha 2017/2018 imekusanya jumla ya Tsh Trilioni 7.87 ikilinganishwa na Tsh Trilioni 7.27 ambayo ilikusanywa wakati wa kipindi hicho hicho kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ikiwa ni ongezeko la 8.46%.
Ripoti ambayo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Richard Kayombo imeeleza kuwa kwa mwezi December 2017 pekee, TRA imekusanya Tsh Trilioni 1.66 ikilinganishwa na makusanyo ya December 2016 ya Trilioni 1.41 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 17.65.
Mnada wa magari 140 ya TRA yaliyotelekezwa bandarini umefanyika leo
BREAKING: TRA kuanza kumchunguza Kakobe, “nina hela kuliko Serikali”