Bodi ya Shule ya Sekondari ya Oysterbay imewaomba wadau wa elimu kujitokeza kuikarabati shule hiyo licha ya kuwa ipo maeneo ya watu wenye fedha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Bernard Mchomvu amewaambia waandishi wa habari kuwa shule hiyo ina madarasa 17, sakafu zimechoka na yanavuja ambapo yanahitajikla mabati 600 kwa ajili ya ukarabati.
“Kama kuna mtu anaweza kusema anachukua darasa hili kwa ajili ya kulikarabati itakuwa nzuri sana kwani tunaogopa kusema leteni hela bali sisi tunataka phisical job ifanyike,“amesema.