Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Hili ndio jina la mtoto wa nne wa Kanye West na Kim Kardashian

on

Zimepita siku chache toka familia ya staa wa muziki wa HipHop Marekani, Kanye West ipokee  mtoto wao wa nne kwenye familia yao na naelezwa kuwa tayari familia hiyo wameshampatia jina mtoto wao wanne aliyezaliwa na mama mbadala May 10,2019.

Inaelezwa kuwa familia ya West wamemuita mtoto wao  Zaburi “Psalm” ambapo hapo awali iliripotiwa kuwa jina la mtoto  huyo ni Robert HarutKanye West pamoja na Kim Kardashian itakuwa ni mara yao ya pili kutumia njia hiyo ya kumpandikiza mama mbadala yaani “Surrogate mother” mtoto wao wa tatu ambaye ni Chicago West alizaliwa kwa njia hiyo pia.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Kim Kardashian aliweka chats alizopata kutoka kwa mume wake Kanye West kuhusu siku ya mama duniani na alimuandikia ‘Siku ya Mama duniani na kuwasili kwa mtoto wetu wa nne, tumebarikiwa kuliko tulivyotegemea’ na Kim Kardashian akaandika caption ‘Psalm West’.

Kwa sasa familia yao inaundwa na  jumla ya watoto wanne akiwemo North, Saint, Chicago na Psalm West. Inaelezwa kuwa Kim Kardashian alipata matatizo ya uzazi baada ya kujifungua mtoto wake wa pili Saint west ndio maana kwa mtoto wao wa tatu na nne wametumia njia mbadala.

VIDEO: ULIPITWA NA  CHUO ALICHOSOMA JUX NCHINI CHINA?, MWALIMU WAKE AFUNGUKA, BONYEZA HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments