Wakati uchaguzi wa kumpata Rais mpya wa FIFA ukitarajiwa kufanyika februari mwakani, Rais wa shirikisho soka Ulaya (UEFA) Michel Platini kesho anatarajiwa kutangaza azma yake ya kuwania urais wa FIFA.
Platini baada ya kuungwa mkono na mashirikisho ya soka kutoka mabara manne atakuwa mgombea wa nafasi hiyo wakati uchaguzi wa shirikisho la soka duniani utakapofanyika februari 26 mwakani.
Raia wa FIFA kwa sasa Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 na anatarajia kustaafu mwezi Februari kutokana na kashfa ya ufisadi katika shirikiso la FIFA.
Na Platini anapigiwa upatu kumrithi.
Baadhi ya wanaomuunga mkono Platini ni pamoja na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, shirikisho la soka kusini mwa Marekani Conmebol,shirikisho la kaskazini, America ya kati na visiwa vya Carebean, Concacaf na la Asia AFC.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.