Filamu ya Kitanzania inayoitwa Still Okay To Date imefanikiwa kushinda Tuzo za Kalasha zinazoandaliwa na Bodi ya Filamu ya Kenya ambazo zimefanyika Nairobi.
Filamu hiyo imeshinda katika kipengele cha Best International Award kilichoshindanisha Filamu kutoka nje ya Kenya ikiwemo Filamu kutoka Uganda na nyingine tatu kutoka Tanzania.
Watayarishaji wa filamu hiyo ni Jerryson Onasaa @code_Jerry na Kefa Igilo @kefa_ig ndio ambao wamepokea Tuzo hizo.
Director wa Filamu hiyo ambayo imeingia sokoni mwaka huu ni Mathew Valerian na imeigizwa na Wasanii kibao akiwemo Elizabeth Chijumba (NIKITA) Tunu Mbegu na Dkt. Issa Mbura.