Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Dorothy Semu na Katibu Mkuu wa Chama Cha NCCR Mageuzi Juju Danda hivi karibuni wamekutana na kufanya mazungumzo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo.
Kamati hii ilimtaka Katibu Mkuu huyo Semu kukutana na Makatibu Wakuu wa vyama vyote vya upinzani ili kujadiliana na kupanga namna bora ya kupigania kwa pamoja misingi ya kidemokrasia.
Katibu Mkuu Semu pia amekwishakutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Chama cha Democratic Party (DP) Joachim Mwakitiga kama maagizo yalivyotolewa.
Musukuma kafunga kampeni kumnadi mgombea Ubunge Songea.