Jana September 6, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikabidhiwa rasmi ripoti za Tume mbili ambazo ziliundwa na Bunge kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma.
Baada ya ripoti hizo kukabidhiwa na kubainika kuwepo kwa baadhi ya vigogo kuhusika katika mikataba iliyosababisha hasara kwa Taifa, watu mbalimbali walipata nafasi ya kuuelezea maoni yao kuhusu waliohusika ambapo miongoni mwa waliopata nafasi hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe na wenzie.
RIPOTI YA MADINI! Kuna Vigogo wengine wametajwa kwenye Ripoti mpya
“Lazima tuchukue hatua kali, kesho namfikishia Rais” – Majaliwa