Ukikaa karibu na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kumekuwa na ripoti mpya kila wakati na kadri zinavyonifikia na mimi nahakikisha hupitwi hata kidogo.
Kama unakumbuka December 03 2015, Rais Magufuli alikutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania na moja ya vitu alivyokosoa na kuonekana kukasirishwa navyo sana ilikuwa ishu ya kubinafsishwa kwa ufukwe wa Coco Beach, Dar es Salaam.
Ripoti imenifikia kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya na Kinondoni Dar es Salaam na baadae kuhamishiwa Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, Mussa Natty amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali.
Kwenye taarifa hiyo kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeonesha sehemu ya tuhuma zinazomkabili Mkurugenzi huyo ni pamoja na usimamizi mbaya uliosababisha barabara za Manispaa ya Kinondoni kuwa chini ya kiwango, ukosefu wa uadilifu na kubinafsisha ufukwe wa Coco Beach pamoja na usimamizi mbovu wa watumishi wa idara za ardhi.
Katibu mkuu ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Jumanne Sagini amesema pamoja na kusimamishwa kwa Natty, anapaswa kurudi kwenye halmashauri ya manispaa ya Kinondoni na kusubiri uchunguzi zaidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE