Urafiki wa karibu uliokuwa kati ya Mwanahipop 50 Cent na Bondia Floyd Mayweather kutokea Marekani unaonekana kuwa na doa ikiwa wawili hao wameonekana kurushiana vijembe kupitia mitandao ya kijamii na wengi kudai kuwa urafiki wao umekuwa wa kupatana na kugombana mara kwa mara.
Floyd Mayweather pamoja na 50 Cent wametumia ukurasa wa instagram kurushiana maneno hayo na safari hii Floyd Mayweather ameulinganisha utajiri wa 50 Cent na saa yake aliyoinunua zaidi ya shillingi Billioni 40 na kumtaka 50 Cent afanye bifu na saa yake lakini sio maisha yake kwasababu hawapo sawa katika maisha.
Kwa mujibu wa mtandao wa google umetaja utajiri wa 50 Cent ambao ni zaidi ya Billioni 45 za Kitanzania ikiwa imezidi Millioni 2 ya thamani ya saa ya Mayweather aliyoinunua mwezi uliopita ikiwa imezungukwa na madini ya almasi.
ULIPITWA? MAMA KANUMBA AFAFANUA KAULI YAKE BAADA YA KUONEKANA AMEFURAHISHWA NA KIFO CHA PATRICK
VIDEO: IDRIS ASEMA “NINAMJALI WEMA HATA INGEKUWA MILIONI 100 NINGELIPA, NINA MPENZI SIWEZI RUDIANA” BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA MWANZO MWISHO