Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi Nyanda tarehe 03/12/2021 alikutana na ujumbe wa jarida la Forbes Afrika uliyoongozwa na Mkurugenzi Mkazi Bi. Bettty Buyu.
Dhumuni la ujumbe huo ni kutangaza vivutio vya utalii na maeneo ya uwekezaji yanayosimamiwa na TAWA kupitia jarida lao maarufu la Forbes Africa.
Katika mazungumzo hayo, Mabula ameeleza kufurahishwa na ujio wa ugeni huo wenye dhamira chanya ya kuitangaza TAWA na juhudi za Serikali katika kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya utalii.
Kwa upande wao Forbes, kupitia kwa Bw. Francesco Forza, ambaye ni mshirika wa mradi wa jarida hilo, amesema Toleo lijalo ni maalumu kwa kuitangaza Tanzania, kutokana na upekee wake katika sekta ya utalii duniani hasa wakati huu wa janga la uviko-19.