Kampuni ya SportPesa ambao ndio wadhamini wakuu wa timu za Simba SC na Yanga wametangaza ujio wa club ya Sevilla ya nchini Hispania kuja Tanzania, ujio wa club hiyo unakuja Tanzania kucheza kati ya Simba SC na Yanga ambao wanadhaminiwa na kampuni hiyo.
Sevilla ambao ni Mabingwa mara tano wa Kombe la UEFA Europa League, hivyo kutokana na ujio wao Tanzania inaonekana waziri wa michezo Dr Harrison Mwakyembe kwa kushirikiana na waziri wa maliasili na utalia Dr Hamis Kigwangalla wameonekana kutaka kutumia fursa timu hiyo ikitua Tanzania waipeleke pia katika vituo vya utalii kuutangaza utalia Tanzania.
Waziri Mwakyembe alitoa taarifa hizo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akizungumzia ujio huo, ambapo Sevilla inakuwa timu ya kwanza ya LaLiga kutua Afrika Mashariki, baada ya mwaka uliopita FC Barcelona kutembelea Afrika Kusini, Sevilla itacheza mechi ya kirafiki na Simba au Yanga May 23 2019 uwanja wa Taifa.
Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23