Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Mchezaji wa Guinea U-17 aliyekuja kucheza AFCON Tanzania, afariki dunia baada ya kurudi kwao

on

Taarifa ya kusikitisha iliyoripotiwa na mtandao wa sportinglife.ng ni kuwa taifa la Guinea limempoteza mwanasoka chipukizi Aly Soumah aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Guinea U-17 kilichokuja Tanzania kwa ajili ya michezo ya AFCON U-17.

Aly Soumah baada ya kurudishwa kwao amepata ajali ya gari katika eneo la Kindia nchini kwao Guine na baadae kufariki, Soumah kwa bahati mbaya alirudishwa nyumbani kwao Guinea mapema baada ya kufeli vipimo vya MRI ambavyo vinatumika kutambua umri wa mchezaji kama kavuka umri wa miaka 17.

Hivyo kutokana na kipimo hicho kumuonesha kuwa kavuka umri alilazimika kurudishwa kwao kabla ya mchezo wa ufunguzi wa AFCON kati ya timu yake ya Taifa ya Guinea katika uwanja wa Chamazi Dar es Salaam dhidi ya Cameroon ambapo katika mchezo huo Cameroon walishinda 2-0.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments