Shirikisho la soka Uganda (FUFA) leo kupitia Rais wa shirikisho hilo Moses Magogo wametoa msaada wa mchele tani 12.5 nchini Uganda kwa ajili ya kugawa katika familia mbalimbali wakati huu wa janga la corona.
FUFA pia imeeleza kuwa sehemu ya tani hizo pia zitaenda kwa wanasoka, viongozi na watu mbalimbali waonaofanya kazi katika taasisi za soka Uganda ambao kwa sasa vipato vyao vimeyumba kutokana na janga la corona.
Shehena hiyo ya mchezo imekabidhiwa katika kitengo maalum cha chakula wakati huu wa janga la corona kupitia ofisi ya waziri mkuu Uganda.