Jumanne ya October 2 2018 Rais wa Auto mobile Association Tanzania (AAT) Nizar Jivan alimkaribisha Kamanda mkuu wa polisi wa kikosi cha usalama Tanzania Fortunatus Muslim ili kuhitimisha na kuwapa vyeti waaalimu waliohitimu mafunzo hayo.
AAT pamoja na Federation Intertnational de Automobile (FIA) wamehitimisha mradi huo uliyokuwa unalenga kuwafaidisha wanafunzi zaidi ya 26000 kwa mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kufanikisha kutoa elimu kwa waalimu 1446 wa kuanzia shule za msingi hadi High School, jumla ya walimu kutoka shule 62 ambao wataenda kuwafundisha wanafunzi kuhusu usalama barabarani.
Kamanda Muslim akiongea mbele ya viongozi na watu mbalimbali akiwemo Rais wa AAT Nizar Jivan na mkurugenzi wa mradi huo Yusuf Ghor, amewapongeza kwa kukamilisha mradi huo kwa ukamilifu na kuwasifia kuwa baada ya kutoa mafunzo wao yameonesha kusaidia na kupunguza ajali za barabarani mkoa wa Dar es Salaam kuanzia 2016-2018.
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga