Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA wamekuwa na utaratibu wa kutambua mchango wa kila mchezaji na makocha waliofanya vizuri katika soka na kuwazawadia tuzo kwa kutambua na kuthamini mchango wao walioutoa katika soka kwa mwaka husika.
Leo Jumatatu ya September 3 2018 FIFA wametangaza majina ya wachezaji watatu watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka, ambapo kwa mwaka huu tumeona zimeingia sura mpya na sio Lionel Messi wa FC Barcelona na kubaki Cristiano Ronaldo wa Juventus ambao ndio walikuwa washindani pekee wenye nguvu.
Kwa mwaka huu mambo yamekuwa tofauti kuanzia tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya hadi leo tuzo ya FIFA, Lionel Messi hayupo katika list hiyo na TOP 3 iliyotangazwa na FIFA wametajwa Cristiano Ronaldo wa Juventus, Mohamed Salah wa Liverpool na Luka Modric wa Real Madrid.
Kukosekana kwa jina la Lionel Messi katika list hiyo hakujawashangaza sana watu wengi kutokana uwezo wake msimu uliopita lakini kubwa wengi wameanza kutabiri kuwa inawezekana huo ndio ukawa mwisho wa utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika soka kwani licha ya Ronaldo kuingia katika kipengele hicho lakini hapewi nafasi ya ushindi sana kama ilivyo kwa Modric.
Kwa upande wa makocha Didier Deschamps wa Ufaransa, Zlatko Dalic na Zinedine Zidane ambaye alikuwa Real Madrid msimu uliopita, tuzo za FIFA zitatolewa katika mji wa London nchini England September 24 2018.
Kitu Mzee Akilimali kaongea kuhusu stori za Yussuf Manji kurudi Yanga SC