Wanachama wa Umoja wa Wabunge wa Kupambana na Malaria na Magonjwa ya Ukanda wa Joto yasiyopewa kipaumbele (TAPAMA & NTD) wanatembelewa na wabunge wenzao kutoka nchini Uingereza na Ujerumani walio wanachama walio katika mapambano ya magonjwa haya yaani APPG (All Parties Parliamentary Group on Malaria and NTD).
Wabunge hawa watakuwepo Nchini kwa mwaliko wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa TAPAMA kwa Ziara ya siku nne kuanzia 16 September mpaka 20 September 2019, Wabunge hawa kutoka Uingereza na Ujerumani wametembelea mkoa wa Kilimanjaro ambapo watafanya mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Anna Mghwira juu ya miradi mbalimbali yenye lengo la kutokomeza malaria.
Akiongea katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amewashukuru umoja wa wabunge hawa kutoka Uingereza, Ujerumani na wenzao wa Tanzania kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kutokomeza ugonjwa wa malaria na magonjwa yasiyopewa kipaombele.
Wakiwa mkoani humo, timu ya Wabunge wawili kutoka Uingereza na wajumbe wa kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi nchini-Hellen Keller na Sight Savers, wametembelea Kituo cha Afya -Karume, Wilaya ya Rombo.
Wakiwa kituoni hapo wageni hao wameshuhudia wananchi waliokusanyika kwa ajili ya kupatiwa huduma za tiba ya macho kutokana na ugonjwa wa vikope, awali wananchi hao walitembelewa na Wataalam wa afya kwenye makazi yao na kuwahamasisha kuhudhuria kliniki na kufanyiwa uchuguzi wa kina.
Zoezi la huduma limehusisha upasuaji mdogo wa macho kwa wagonjwa waliogundulika kuwa na ugonjwa huo wa vikope. Zaidi ya wagonjwa 30 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo, zoezi hili litaendelea hadi kesho, mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, TAMISEMI na Kilimanjaro Center for Community Ophthalmology (KCCO) kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa Commonwealth.
Katibu wa TAPAMA Dr Raphael Chegeni amesema kuwa lengo na Madhumuni ya ziara hii ni kutoa Nafasi kwa Wawakilishi Wabunge wa Umoja wa APPG wa Uingereza na Ujerumani kutembelea nchi yetu Tanzania na kukutana na wenzao wawakilishi wa TAPAMA ili kuweza kupata fulsa ya kujadili kwa pamoja njia za kushirikiana na kuweka mikakati ya pamoja ya kuisadia Tanzania kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030 na Magonjwa ya Ukanda wa Joto yasiyopewa kipaumbelele (NTD).
Pia watakutana na Waziri wa Afya na Management ya Wizara katika mpango wa Kutokomeza Malaria Tanzania (NMCP) kwa Mazungmzo Mazungumzo ya Muda mfupi tarehe 19th September 2019, Mjini Dodoma. Kujadili Changamoto ambazo Wizara ya Afya inazokumbana nazo Katika harakati za kutokomeza Malaria na NTD Tanzania na nini kifanyike kwa usadizi kutoka Serikali na Watu wa Uingereza kupitia Mpango wake wa Maendeleo Kimataifa (DFID.
Watatembelea Miradi kadhaa ya Malaria na NTD (Neglected Tropical Disease) iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa Tanzania kwa Ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia DFID na Global Fund.
VIDEO: Moja kati ya magoli ya marehemu Jeba, hili liliwaumiza wana-Simba 2016