Hivi ndivyo Bobi Wine alivyosikiliza dhamana yake siku ya jana ya May 2,2018 mahakamani baada ya kutoweza kufika mahakamani kwa sababu za kiusalama hivyo ilitumika njia ya video akiwa gerezani na kuonekana moja kwa moja mahakamani.
Inaripotiwa kuwa Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine amepatiwa dhamana jana Mei 2 na kupewa masharti magumu kulingana na umaarufu alionao ambapo Mahakama imemkataza kuhusika katika mikusanyiko au maandamano.
Bobi Wine alishtakiwa kwa kushiriki katika maandamano ya ‘haramu’ mwaka jana 2018 ya kupinga kodi ya kutumia mitandao ya kijamii maarufu Uganda kama OTT, inaelezwa kuwa aliandaa maandamano ya umma kinyume na sheria, na alizuiwa siku ya Jumatatu katika kituo cha polisi cha Naggalama kwa mujibu wa taarifa ya polisi.
VIDEO: PIERE KAZUNGUMZA KUZUSHIWA KIFO, KUMPA JOKATE MADAWATI YA MILLIONI 5