The Game alikuwa na noma na Polisi mwezi March 2015, video ikanaswa na kusogezwa Youtube.. Baadae Polisi waliona hii wasiiache, story kwenye headlines ni kuhusu jamaa kukamatwa na Polisi japo kosa alilifanya muda mrefu uliopitwa.
Rapper huyu amefunguliwa mashitaka na Polisi wa Los Angeles baada ya kuingia kwenye utata na polisi wakati wanacheza Basketball na kisha kumpiga ngumi polisi huyo tukio ambalo watu walilinasa kwenye video na baadae likarushwa kwenye mtandao wa YouTube.
Japo video hio ina muda wa miezi mitatu toka irushwe Youtube, Police wamesema kwamba wamefungua mashitaka kutokana na video hiyo kusambaa Youtube alafu watu wakawa kama wanawadharau Polisi kwa kutomfanya chochote jamaa.
Baada ya kufunguliwa mashtaka, The Game aliachiwa saa chache baadae kwa dhamana.
Hii ndio video inayoonesha tukio la The Game kumpiga Polisi.
https://www.youtube.com/watch?v=Mw6huJMZYJM
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.