Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 May 18 2017 katika uwanja wa Stade de Amitie Libreville Gabon iliingia uwanjani kucheza game yao ya pili ya Kundi B katika michuano ya Afrika vs Angola ambapo mwisho Serengeti Boys ilishinda 2-1
AyoTV na millardayo.com zilipata nafasi ya kukutana Daktari wa Serengeti Boys ambaye anahusika kusimamia afya za Wachezaji akakubali kutuambia aina za vyakula ambavyo Madaktari wamevikataza visitumike hasa kipindi hiki cha mashindano.
“Unaporudiarudia kutumia chakula chenye mafuta mengi mshipa wa damu unasaizi yake ile saizi ya mshipa wa damu kupeleka damu inapunguzwa na mafuta yanayoganda kando’
‘Ikiwa hivyo unapokuwa mchezoni kuna uwezekano ikatokea kwa bahati mbaya mafuta haya yakatoka na kwenda kuziba mzunguko wa damu mbele na pia kuchoka haraka na kushindwa kucheza kwa muda mrefu ” – Dr Gilbert
VIDEO: Tazama hapa chini mazoezi ya Serengeti Boys Gabon